Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA 07,SEPT.2018 SAA 03:30 USIKU
Uongozi wa klabu ya Simba umewataka mashabiki wake na watanzania kwa
ujumla kuipa sapoti Taifa Stars ambayo inacheza
kesho dhidi ya Uganda
kuwania tiketi ya kufuzu kuelekea AFCON 2019.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wake, Haji Manara, amesema watanzania wote
wanapaswa kuwa kitu kimoja kwa kuonesha utaifa na uzalendo kwa Stars
ambayo itakuwa inaiwakilisha nchi.
Aidha, Manara amesema atawashangaa mashabiki baadhi wa Simba ambao
wataipa sapoti Uganda kutokana na kuondolewa kwa wachezaji wake 6 kwenye
kikosi cha Stars kutokana na kuchelewa kufika kambini akieleza kuwa ni
sababu ambayo haina maana.
Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu Ibariki Taifa Stars.
BOFYA CHINI KUSIKILIZA
0 Comments