Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.FEB 28.2016 SAA 12:55 JIONI
Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb), ametangaza Kamati ya watu 10
watakaohamasisha kuwaunganisha Watanzania kwa pamoja ili kuichangia timu ya Tanzania
ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys.
Mheshimiwa Nape alitangaza kamati
hiyo itakayoongozwa na Mtangazaji mkongwe wa habari na Mpira wa miguu nchini,
Charles Hilary mbele ya wanafamilia ya mpira wa miguu waliohudhuria kongamano
ya kujadili juu ya ushiriki wa Tanzania katika michuano ya kimataifa.
Mada ilikuwa ni Tanzania kushiriki
michuano ya Olimpiki Tanzania, lakini kwa kuwa kuna jambo la usoni la timu ya
Serengeti Boys kucheza fainali za Kombe la Dunia huko Gabon kuanzia Mei 21,
mwaka huu, Waziri Nape atakatangaza kamati ya kuhamamsisha ili Watanzania kwa
pamoja waweze kuchangia.
Akitangaza kamati hiyo, Nape alisema
kwamba Katibu wa Kamati hiyo atakuwa Mwesigwa Selestine ambaye ni Katibu Mkuu
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakati wajumbe ni Mtangazaji wa
Radio ya EFM, Maulidi Kitenge; Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel
Tanzania, Beatrice Singano na Mrembo wa Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu.
Pia wamo Mkurugenzi wa Habari katika
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas; Mkurugenzi wa Global
Publishers Limited, Eric Shigongo; bosi wa radio Clous, Ruge Mutahaba pamoja wa
wasanii wa kizazi kipya Diamond Platnums na Ally ‘King’ Kiba.
Pamoja na hayo, katika kongamano hilo
na wadau wa soka wadau ikiwamo Serikali iliridhia kuwa mshiriki wa karibu kwa
kila hatua kuanzia Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya timu za taifa, Kamati ya
Hamasa kwa lengo la kupanga pamoja na kushirikiana kwa pamoja.
Wameazimia kuwa na chanzo cha fedha
cha kueleweka ili kufanikisha program mbalimbali za timu za taifa ikiwamo ya
U23 ambayo inatakiwa kushiriki kwenye michuano ya Olimpiki. Serikali imepanga
kuwa pamoja badala ya kile kinachoitwa kudandia matokeo mafanikio bila
kushiriki maandalizi.
Kadhalika wameazimia mpira kuwa jambo
la nchi ili hamasa inayotangazwa iguse wadau wote kwa maana ya Watanzania wote.
Pia chanzo cha kupata vipaji kiwe pia
kutoka mashuleni (Umitashumta na Umiseta) ambako Mheshimiwa Waziri Nape mbali
ya kuthibitisha kuwa mwaka huu itafanyika tofauti na mwaka jana, pia aliagiza
kuwa isiwe kama matamasha.
0 Comments