Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.FEB 28.2016 SAA 12:57 JIONI
Timu nne vinara wa Ligi
Daraja la Pili kutoka makundi manne, zinatarajiwa kuanza kupambana kesho
Jumatano - Machi mosi,
mwaka huu ‘Play off’ kutafuta timu Tatu Bora,
zitakazopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2017/2018.
Timu hizo zilizofanya vema
ni pamoja na JKT Oljoro ya Arusha, Cosmopolitan ya Dar es Salaam, Mawenzi ya
Morogoro na Transit Camp ya Shinyanga. Ziliibuka vinara katika makundi yao.
Ratiba iliyotolewa na Bodi
ya Ligi, inaonesha kuwa Ratiba ya Nne Bora itakuwa na raundi mbili ambazo kwa
pamoja zitacheza kwa mwezi mmoja kuanzia Machi mosi hadi Aprili mosi, mwaka
huu.
Raundi ya kwanza itaanza
siku ya Machi mosi, mwaka huu ambako kutakuwa na mechi mbili ambazo Transit
Camp itacheza na Mawenzi kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati
Cosmopolitan itacheza na JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo,
Machi 5, mwaka huu kutakuwa pia na michezo miwili ambako JKT Oljoro itacheza na
Transit Camp kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Mawenzi
Market itacheza Cosmopolitan kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Machi 12, mwaka huu JKT
Oljoro itacheza na Mawenzi Market kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini
Arusha wakati Cosmopolitan itacheza na Transit Camp kwenye Uwanja wa Karume,
Dar es Salaam.
Raundi ya Pili ya ligi hiyo,
itaanza Machi 18, mwaka huu kwa timu za Mawenzi Market itacheza na Transit Camp
kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati siku hiyo, JKT Oljoro itacheza
na Cosmopolitan katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Machi 25, mwaka huu
Cosmopolitan itapambana na Mawenzi Market kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini
Dar es Salaam ilihali Transit Camp itacheza na JKT Oljoro Uwanja wa CCM
Kambarage mjini Shinyanga.
0 Comments