Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.DEC 02.2016 SAA 01:00USIKU
Raundi
ya Tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam 2016 (Azam Sports
Federation Cup 2016) in atarajiwa
kuendelea kesho Desemba 3, 2016 kwa
michezo minne itakayokutanisha timu nane zilizofanya vema raundi ya
kwanza na pili.
Michezo
ya kesho ambayo itakuwa mubashara (live), kupitia chaneli mbalimbali
za Kituo cha Televisheni cha Azam ‘Azam Tv’ itakuwa ni kati ya Mtwivila
ya Iringa na Jangwani ya Rukwa mchezo unaotarajiwa kufanyika mkoani
Iringa wakati Stand ya Bagamoyo itacheza na Mbuga ya Mtwara kwenye
Uwanja wa Mabatini, ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Stand Misuna ya Singida inatarajiwa kuwa wenyeji wa Kabela City ya
Shinyanga kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati Mulusagamba ya
Kagera na Baruti ya mkoani Mara zitachuana kwenye Uwanja wa Kaitaba,
Bukoba mkoani Kagera katika mfululizo wa mechi hizo.
Mechi hizo zitatoa timu nne bora kutoka mabingwa wa Mkoa na hivyo
kuungana na timu 24 za Ligi Daraja la Pili kwa michezo ya hatua ya
raundi ya nne na tano kutafuta timu nane bora zitakazosonga mbele
kukutana na timu za Daraja la Kwanza.
0 Comments