Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.DEC 07.2016 SAA 12:44 JIONI
Kamati ya usimamizi na uendeshaji imempa adhabu ya Kumfungiwa miezi
mitatu Katibu Mkuu wa Rhino Rangers,
Dickson Cyprian Mgalike kwa kosa la
kuidanganya kamati kwa kutoa taarifa potofu katika barua aliyoiandikia
Bodi ya Ligi.
Hapo awali, Kamati ilimuadhibu Mchezaji Sameer Mwinyishere kwa kosa la kumrushia chupa ya maji mwamuzi.
Katibu aliandika barua kusema kwamba Sameer hakufanya kosa hilo na
alimtaja mchezaji Yusuf Mputa kwamba ndiye aliyefanya kitendo cha utovu
wa nidhamu kwa kumrushia Mwamuzi chupa ya maji.
Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji kwa kushirikiana watendaji wa Bodi
ya Ligi ilifanya uchunguzi na kubaini mchezaji Yusuph Mputa hakuwepo
kwenye Orodha ya Wachezaji wa siku hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa
kufuata kanuni ya 41(6).
0 Comments