Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.DEC 07.2016 SAA 01:00 USIKU
Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Vijana wa Tanzania wenye umri wa
chini ya miaka 15, kesho Desemba 8, 2016 inaanza rasmi
ziara ya mkoani
Morogoro ambako watakuwa na mchezo wa kirafiki kesho jioni na keshokutwa
asubuhi.
Vijana hao 22, walioko kambini kujiandaa Dar es Salaam wanajiandaa na
mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Shelisheli unaotarajiwa
kufanyika Desemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao una baraka za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA), umepangwa kufuata taratibu zote za kimataifa ikiwa ni
pamoja na kupigiwa Nyimbo za Taifa kwa timu zote sambamba na kupandisha
Bendera za Mataifa husika.
Mara baada ya Morogoro itakayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, timu
hiyo itarejea Dar es Salaam jioni ya Desemba 9, 2016 kujiandaa na safari
ya Zanzibar Desemba 11 ambako itakuwa na michezo miwili mingine ya
kirafiki.
Zanzibar itacheza na Kombaini ya timu ya Vijana wa Zanzibar Desemba
12, 2016 kabla ya kurudiana Desemba 14, mwaka huu na timu hiyo na
Kombaini kabla ya kurejea Bara Desemba 15, kujiandaa na mchezo kirafiki
wa kimataifa dhidi ya Shelisheli.
Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu wa timu ya vijana wenye umri
wa chini ya miaka 14, Oscar Mirambo anayepata ushauri kutoka kwa
Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana, Kim Poulsen kinaundwa na
makipa ni Shaban Hassan Kimwaga na Abdulatif Noor Lema.
Walinzi ni Kareem Bakari Mfaume, Asante Hamis Bwatam, Rashid Hamisi
Rashid, Moris Michael Njako, Harubu Juma Tanu, Cosmas Lucas Jakomanya,
Salim Abubakar Lupepo na Dastan Daniel Matheo.
Viungo ni Edson Jeremiah Mshirakandi, Jonathan Raphael Kombo,
Alphonce Mabula Msanga, Erick Boniface Bunyaga, Gssper Godfrey
Gombanila, Sabri Dahari Kondo na washambuliaji ni Jafari Juma Rashid,
Ludaki Juma Chasambi, Steven Emmanuel Sodike, Michael Mussa Mpubusa na
Edmund Geofray John.
Timu hii inaundwa na vijana ambao TFF iliwakusanya tangu 2014 na
kuwaunganisha kwa pamoja katika Shule ya Msingi na Sekondari ya Kukuza
Vipaji ya Alliance iliyoko Mwanza. Mbali ya kutoa elimu ya msingi na
sekondari, pia Alliance inatoa elimu ya awali kwa watoto wa kuanzia umri
wa miaka miwili hadi sita.
Timu hii inaandaliwa kuja kwa time mpya ya Vijana wenye umri wa chini
ya miaka 17 ambao watashiriki fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa
vijana mwaka 2019 ambako Tanzania imeteuliwa na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) kuwa mwenyeji. Kambi itavunjwa Desemba 18, mwaka huu.
0 Comments