Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.DEC 07.2016 SAA 12:35 JIONI
Waamuzi waliochezesha mchezo namba 49 kati ya Yanga na Simba, Martin
Saanya na Samweli Mpenzu wametolewa kwenye ratiba ya
Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, huku suala lao likipelekwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili
ishughulikie tatizo lao kitaalam.
Maamuzi hayo yamefanyika baada ya Kikao cha Kamati ya Usimamizi na
Uendeshaji ya Bodi ya ligi, kuwaita na kuwahoji na kuangalia mkanda wa
mchezo husika. Kamati imebaini mapungufu mengi ya kiutendaji
yaliyofanywa na waamuzi hao, na hivyo kuitaka kamati ya waamuzi
ishughulikie.
Pia Mwamuzi Rajabu Mrope aliyechezesha mchezo namba 108 kati ya Mbeya
City na Yanga naye ametolewa kwenye Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu
2016/2017 na kurudishwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili waweze kumpangia
daraja lengine la uamuzi.
Mrope alitiwa hatiani kwa kosa la kutojiamini mchezoni na kwenye uamuzi wake na kushindwa kuudhibiti mchezo.
Miongoni mwa matatizo ya mwamuzi huyo ni kukubali goli, kisha kukataa
na mwisho kukubali tena hali iliyoonyesha kutokujiamini na kusabisha
mtafaruku mkubwa katika mchezo huo.
Katika ligi ya Daraja la kwanza, Mwamuzi Thomas Mkombozi
aliyechezesha mechi namba 15B kati ya Coastal Union na KMC ameondolewa
kwenye orodha ya waamuzi kutokana na kushindwa kuudhibiti mchezo na
kutoshirikiana na wasaidizi wake.
Adhabu hiyo ametolewa baada ya Kamati ya usimamizi na uendeshaji wa
ligi kuwaita waamuzi wa mchezo huo na kufanya mahojiano nao na kugundua
Mkombozi alikuwa na maamuzi mengi bila umakini na hakushirikiana
kiufundi na wasaidizi wake. Kutokua makini kulisababisha mchezo huo
kumalizika kwa vurugu.
Pia Klabu ya Coastal Union imepewa adhabu ya kucheza bila ya
mashabiki kwa mechi mbili za nyumbani na mechi moja ya nyumbani kuchezwa
uwanja wa ugenini kwa kosa la mashabiki wa timu hiyo kumshambulia
Mwamuzi Thomas Mkombozi na kumsababishia majera ha maumivu makali.
kuhusu Mwamuzi Ahmed Seif, Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya bodi
ya Ligi, imemfungulia na kumtoa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi kuu
mwamuzi huyo aliechezesha mchezo namba 28 kati ya African Lyon na Mbao
FC. hivyo, Mwamuzi Ahmed Seif atarudishwa kwenye kabati ya waamuzi ili
apangiwe majukumu mengine.
0 Comments