Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.OCT.21,2016 SAA 01:26 USIKU
Mwenyekiti
wa klabu ya Young Africans Yusuf Manji amewataka wanachama wa klabu hiyo
kujitokeza kwa wingi katika mkutano
mkuu wa dharura ambao umepangwa kufanyika
mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa Kaunda jijini Dar es salaam.
Manji
amesema kila mwanachama wa Young Africans mwenye haki ya kuhudhuria mkutano huo
wa dharura anapaswa kufika bila kuhofia vitisho vinavyoendelea kutolewa na
baadhi ya watu ambao wameonyesha kupingana na dhamira ya mabadiliko inayotaka
kufanyika klabuni hapo.
Amesema
katika mkutano huo atakuwa muwazi na atatoa uhuru kwa wanachama kuwa na haki ya
kufanya maamuzi katika masuala ambayo yatahitaji ridhaa yao kwa kupiga kura ya NDIO
ama HAPANA.
Katika
hatua nyingine suala la Katibu wa Kamati ya Muafaka ya Wazee wa Yanga, Ibrahim Omar
Akilimali likaibuka kwenye mkutano wa Yusuf Manji na waandishi wa habari
kufutia taarifa ambazo zimesambazwa katika mitandao ya kijamii kuhusu uhalali
wa uanachama wa mzee huyo ambaye juzi alijitokeza hadharani na kupinga mpango
mabadiliko ambao huenda ukaafikiwa katika mkutano mkuu wa dharura wa wanachama
siku ya jumapili.
0 Comments