Ticker

6/recent/ticker-posts

TFF YATOA MUDA KWA YANGA SC

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 9,2016 SAA 11:19 JIONI

Shirikisho la soka nchini TFF, limetoa muda wa siku mbili kwa viongozi wa Young Africans kuwasilisha sababu kwa njia ya

maandishi (barua) za kushindwa kukamilisha zoezi la usajili wa wachezaji kwa njia ya TMS kama kanuni za ligi kuu ya soka Tanzania bara zionazotaka.

TFF juzi walithibitisha hawajapokea usajili wa wachezaji wa Young Africans kwa njia ya mtandao, halia mbayo huenda ikawasababishia matatizo makubwa kutoka FIFA, likiwepo suala la kushushwa daraja.

Katibu mkuu wa TFF Celestine Mwesigwa, hii leo amekutana na waandishi wa habari na kusema kwamba sababu za kimaandishi ambazo zitawasilishwa na mabingwa hao wa Tanzania bara ndizo watakazo zitumia kwa ajili ya kuwaombea utetezi FIFA, ili kuona kama watapata uwezekano wa kufunguliwa kwa mtandao wa usajili wa wachezaji ambao tayari umeshafungwa tangu usiku wa kuamkia jumapili.

Mwesigwa amesema mbali na Young Africans pia zipo klabu nyingine za ligi daraja la kwanza (Coastal Union) ambazo zimeshindwa kutimiza masharti ya kikanuni ya kufanya usajili wa wachezaji wakati wa dirisha la usajili ambalo lilifunguliwa rasmi June 15 na kufungwa Agosti 06.


Hivyo sasa klabu zote ambazo hakuzituma usajili wake, hazina budi kuandaa utetezi utakaokwenda TFF ambao utatumwa FIFA yenye mamlaka ya kufungua dirisha, na utetezi huo ukikataliwa timu husika inabidi ishuke daraja ambalo halimo kwenye usajili wa mfumo wa TMS.

TFF kwa sasa inasuburi barua ya utetezi wa klabu ambazo hazikukamilisha zoezi la usajili ili iutume FIFA. Sambamba na hilo TFF inatathimini mwenendo mzima kisha itatoa taarifa kwa FIFA ili kuangalia namna gani ya kushughulikia maeneo yaliyokuwa na upungufu kwa sasa na baadaye.


KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments