Pogba hii leo siku ya Jumanne kakamilika rekodi ya dunia ya uhamisho wa £ 89m kutoka Juventus kwenda Manchester United, Kiungo huyo wa kati amerejea miaka minne baada ya kuondoka United na kwenda Juventus kwa £1.5m mwaka 2012.
Pogba mwenye umri wa miaka 23 alisema hana shaka na Mourinho na ni mtu mzuri kwa kusaidia wachezaji
Niliongea na wachezaji wengi wakati akiwa Madrid," "nilizungumza na (Alvaro) Morata, (Raphael) Varane Na wote waliniambia kuwa ni kocha kwa ajili yangu, ataboresha mengi, kwa sababu yeye hufanya kazi kwa bidii.
Paul Pogba anasema huu "ndio wakati bora zaidi wa kurejea Old Trafford" na kwa sasa afikiria atavyocheza uwanjani na jinsi ya kushinda mataji na kuwa bora.
Pogba alicheza mechi saba wakati akiichezea kwa mara ya kwanza akiwa United na kusaidia klabu hiyo katika kikosi cha chini ya U18 kunyakuwa FA Cup ya Vijana mwaka 2011.

0 Comments