![]() |
| Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Mohamed Enterprises, Mohamed Dewji “Mo” akikabidhi hundi ya shilingi milioni 100 kwa rais wa klabu ya Simba Evans Aveva (PICHA NA dewjiblog.com) |
Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Mohamed Enterprises, Mohamed Dewji “Mo” hii leo ametimiza ahadi ya kusaidia sehemu
ya usajili wa klabu ya samba kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 100.
“Mo” aliahidi kuchangia sehemu ya fedha za usajili wa klabu hiyo mwishoni mwa juma lililopita alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mpango wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshwaji ambao tayari umesharidhiwa na wanachama kupitia mkutano mkuu.
Kufuatia hatua hiyo, rais wa klabu ya Simba amemshukuru Mohamed Dewji kwa kujitoa kwa mapenzi yake ya dhati kusaidia fedha za usajili ambazo kwa kiasi kikubwa ameahidi zitaelekezwa kwa mchezaji kutoka nchini Ivory Coast.
Katika hatua nyingine Evance Avave amekanusha taarifa za kuwa kinara wa kupinga mabadiliko ya mfumo wa uendeshwaji wa klabu ya Simba kama ilivyosemwa jana na Mohamed Dewji alipozungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kuwashukuru wanachama wa Msimbazi.
Wakati huo huo Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Mohamed Enterprises, Mohamed Dewji “Mo” amesema alikua na mipango mizuri ya kuibiresha Simba endapo mchakato wa mabadiliko ungewahi kupitishwa.
Amesema dhumuni lake lilikua ni kufuata taratibu za usajili kama ilivyo kwenye klabu nyingine barani Afrika na duniani kwa ujumla, lakini kutokana na mchakato huo kuridhiwa mwishoni mwa juma lililopita bado anaamini jambo hilo mhuenda akaanza kulifanyia kazi msimu ujao.

0 Comments