Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 21,2016 SAA 12:35 JIONI
Hii leo Timu ya Taifa ya vijana chni ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys imefanikiwa kuchomoka na ushindi wa mabao 2 kwa 0
dhidi ya Timu ya vijana ya Afika Kusini (Amajimbos) na kufuzu hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Afrika mwakani Madagascar, mchezo huo ulipigwa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamanzi, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Dakika 33 Mohamed Rashid Abdallah aliiandikia Serengeti Boys bao la kwanza.
Ally Ng'anzi wa Serengeti Boys alipewa kadi nyekundu. Alionywa awali kadi ya njano, akaonywa tena kwa kadi ya njano kabla ya mwamuzi Noiret Bacari kutoka Comoro kumwadhibu kwa kadi nyekundu dakika 45.
Mpira ukaenda mapumziko Serengeti Boys ikiwa mbele kwa bao 1-0.
Dakika ya 85 Muhsin Makame aliipiga Amajimbos bao la 2,Krosi ya Mohammed Abdallah.
Mpira ukaisha. Serengeti Boys 2, Amajimbos 0. kwa maana hiyo Tunasonga mbele kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya kutoka sare ya mabao 1-1 wiki mbili zilizopita.
Serengeti Boys sasa itacheza na ama Namibia au Congo Brazaville Septemba, mwaka huu.

0 Comments