Wadhamini wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, kampuni ya mawasilino ya Vodacom, hii leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa
klabu 16 zitakazoshiriki ligi hiyo msimu wa 2016/17 ambao umepangwa kuanza kuunguruma Agosti 20.
Kabla ya zoezi la kukabidhi vifaa hivyo, Vodacom walitumia nafasi ya kuonyesha jezi zitakazotumiwa na klabu zote za ligi kuu ambapo wahusika walipita mbele ya waandishi wa habari na kuonyesha kwa umakini mkubwa.
Meneja mauzo wa kampuni ya Vodacom Nandi Mwiyombela aliwaambia waandihi wa habari kuwa, vifaa vya michezo kwa ajili ya klabu za ligi kuu vimewagharimu zaidi ya shilingi milion 500 na vipo katika ubora wa hali ya juu.
Amesema kutokana na ubora wa vifaa walivyo vigawa hii leo, wanatarajia kuona timu zikishindana kwa ari kubwa na mwishoni mwa msimu bingwa apatikane baada ya kupambana vilivyo.
Naye afisa mtendaji wa bodi ya ligi (TPL Board), Boniface Wambura ameushukuru uongozi wa kampuni ya Vodacom kwa kukamilisha sehemu ya makubaliano ya udhamini wa ligi kuu kwa kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki.
Amesema hali hiyo inaendelea kudhihirisha umakini wa kampuni hiyo wa kuhakikisha ligi kuu ya soka Tanzania bara inaendelea kuwa na ushindani mkubwa pamoja na kukuza viwango vya wachezaji.
Katika hatua nyingine Boniface Wambura amethibitisha matumizi ya uwanja wa Uhuru katika msimu huu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, baada ya maboresho ya uwanja huo kukamilika kwa asilimia 100.
Wambura amesema tayari wameshapata uhakika kutoka wizarani kuhusu kuanza kutumika kwa uwanja huo ambao upo pembezoni mwa uwanja wa taifa, hivyo kuna baadhi ya michezo italazimika kuchezwa uwanjani hapo.
Wakati huo huo afisa habari wa klabu ay Ruvu Shooting Masau Bwire alizungumza kwa niaba ya klabu shiriki za ligi kuu msimu wa 2016/17 na kutoa shukurani kwa wadhamini, huku akitosisitiza kanuni na taratuibu za ligi kufuatwa mara baada ya kipyenga kupulizwa Agosti 20 mwaka huu.
ANGALIA PICHA


























0 Comments