Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:MGOSI AWATOA MACHOZI WANASIMBA LEO TAIFA,AWAANGA RASMI KATIKA SARE NA URA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG 14,2016 SAA 01:23 USIKU

Aliyekuwa nahodha wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi hii leo AUG 14,2016 amewaaga rasmi  mashabiki wa klabu ya simba baada
ya kustaafu rasmi soka .

Mgosi alitumia nafasi hiyo kuwaaga mashabiki katika mchezo wa kirafiki wa Simba Dhidi ya URA mchezo uliomalizika kwa sare ya Bao 1 - 1 uliopigwa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mgosi aliyeungana na familia yake kusheherekea mafanikio yake yake na Simba,alicheza dakika tatu za kipindi cha kwanza kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Jamal Mnyate.kipindi anatoka Mgosi aliinama na kuubusu mpira,kisha akavua kitambaa cha unahodha na kumpatia Jonas Mkude.

Mgosi kwa sasa anakuwa Meneja wa Simba SC.
Mabao yote yalifungwa kipindi cha kwanza,bao la URA lilipatikana dakika ya 19 kupitia kwa Nkugwa Eklanah na bao la kusawazisha la Simba SC likifungwa dakika ya 32 na Nahodha mpya, Jonad Gerald Mkude

ANGALIA PICHA 



Mgosi kawa Meneja wa Simba SC sasa.







 

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments