Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF)
limepania kutoa kipaumbele katika masuala ya waamuzi na wanawake kwa
kuanzisha madawati ya kudumu katika Kurugenzi ya Ufundi.
Hapo awali madawati ya wanawake na waamuzi yaliendeshwa na watumishi wa kujitolea (Volunteers) au wa muda (Part timers).
Akizungumza na www.tff.or.tz,
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliamsha changamoto mbalimbali
za soka la wanawake miongoni mwanzo ikiwa ni uibuaji na uendelezaji
vipaji, Timu ya Taifa, mafunzo katika taaluma mbalimbali, ligi za
wanawake na masoko kwa bidhaaa (products) za soka la wanawake.
Kuhusu waamuzi, Katibu Mkuu alilielezea eneo hili
kama lenye changamoto nyingi hasa hasa katika kupata waamuzi na viwango
vya Kimataifa.
Wakati huohuo, TFF inatarajia kuimarisha Kurugenzi yake ya masoko ambako sasa ataajiriwa Mkurugenzi wa masoko na habari.
Lengo hasa ni kuendana na halihalisi ya uendeshaji
mpira duniani ambako masoko, habari na mahusiano ya Kimataifa yamekuwa
funguo za kupata rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya mchezo wa soka.
Lengo ni kuhakikisha rasilimali za kuendesha
mpira wa miguu zinatokana na mpira wa miguu na vilevile kuhakikisha
wadau wanapata habari sahihi kwa wakati muafaka “ Alisema Mwesigwa
Selestine”
Kwa nafasi za kazi katika TFF tembelea tovuti yao www.tff.or.tz au waandikie ili utumiwe tangazo kwa barua pepe tanfootball@tff.or.tz
0 Comments