Ticker

6/recent/ticker-posts

TAARIFA YA AZAM TV KUONESHA TENA MECHI LIGI KUU TANZANIA BARA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY 12,2016 SAA 07:08 USIKU  
Shirikisho la soka nchini TFF hiii leo limeingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya Azam Media Ltd ambayo imeshinda tenda
ya kuonyesha michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara nyingine tena.

Udhamini huo wa miaka mitao una thamani ya Kihistoria ya shilingi Bilioni 23 ambazo zitakwenda kuzinufaisha klabu za ligi kuu pamoja na shughuli zingine za ligi hiyo ambayo inaendelea kujizoela umaarufu katika ukanda wa Afrika mashariki.
Katibu mkuu wa TFF Celestin Mwesigwa ndiye aliyemuwakilisha rais Jamal malinzi katika kusaini mkataba huo, huku upande wa Azam Media Ltd ukiwakilishwa na Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Tido Muhando.

Mwesigwa amesema hatua kubwa iliyopigwa na kampuni ya Azam Media Ltd ya kuonyesha kwa ufasaha michezo ya ligi kuu kupitia mkataba uliomalizika, ndio imekua chachu ya kujiongeza na kuwasilisha zabuni nzuri ambayo imeshindwa kuleta ushindani kwa makampuni nyingine.


Kwa upande wa Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Tido Muhando amesema wanaamini kushindwa kwao kumetokana na uzoefu walioupata katika hatua za kuutumikia mkataba wa awali ambao uliwawezesha kuonyesha michezo mingi ya ligi ya Tanzania bara katibu katika kila uwanja.

Amesema mbali na hilo, pia wanaamini ubora na utendaji wao kazi pamoja na kuwa na vifaa vyema ubora pia kumechangia kufanikisha azma ya kushinda tenda ya kusaini mkataba mpya na shirikisho la soka nchini TFF.


KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments