Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Moses Nnauye akionesha picha iliyocholwa papo hapo na msanii Cloud Chatanda picha na dewjiblog.com |
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Moses Nnauye hii leo amezindua fursa ya sanaa na utamaduni kwa
watanzania pamoja na ukanda wa Afrika mashariki Afrika mashariki.
Nape ametumia nafasi ya kuzindua tamasha hilo lililoandaliwa na British Council kwa kuwataka wasanii nchini pamoja nan chi za Afrika mashariki, kutumia nafasi walizonazo kujiendeleza.
Hata hivyo Nape amekiri kuwepo kwa changamoto katika sekta ya sanaa nchini, lakini ameahidi kutumia nafasi aliyonayo, ili kuwasaidia wasanii ambao wana kiu ya kufanya vyema kitaifa na kimataifa.
Baada ya kutoa nasaha hizo, Nape Nnauye alipata nafasi ya kuonyesha kipaji chake cha kuimba na kupiga Gita.
SIKILIZA HAPA
WWakati huo huo msanii wa uchoraji Cloud Chatanda amepongeza hatua ya Nape Nnauye kukubali kiitikia wito wa kufungua tamasha hilo, na anaamini hatua hiyo inafungua ukurasa mwingine wa serikali kuendelea kuwathamini wasanii nchini kote.
0 Comments