Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY 15,2016 SAA 09:36 USIKU
Kamati
ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti, Richard
Sinamtwa imebaini kasoro kwa Abajalo FC
kumtumia mchezaji Laurent E.
Mugia hivyo kuamua kumfungia mchezaji huyo kwa kipindi cha mwaka mmoja
kwa mujibu wa kanuni ya 36 (16) toleo la mwaka 2014 la Ligi Daraja la
Pili kwa kosa la kuchezea klabu mbili katika msimu mmoja.
Kwa kuwa kanuni za Ligi Daraja la Pili mpaka Ligi
Kuu zina upungufu unaofanyiwa mapitio pale kiongozi wa timu anapofanya
udanganyifu wa usajili wa mchezaji bila kumshirikisha mchezaji, Kamati
sasa imelazimika kutumia kanuni za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF), Ibara ya VII (10) ikinukuu:
“A team which will have committed a fraud on the
identity of player or which will have allowed a suspended or
non-qualified player to take part in match shall, lose the match and
shall be completely eliminated from the competition as soon as the
incriminating fact are clearly established by CAF organizing committee.”
Mwisho wa kunukuu.
Kwa maelezo hayo, timu
ya Abajalo FC inanyang’anywa pointi sita. Timu za Pamba SC na The Mighty
Elephant wanapewa pointi tatu kila timu na magoli matatu.
Kamati inaagiza Sektretarieti kuwachukulia hatua
na kuwapeleka katika vyombo vya Serikali viongozi wote wa timu ya
Abajalo walioshiriki kubadilisha jina la mchezaji alilotumia akiwa na
timu ya Kagera Sugar ili kufanikisha usajili wao na pia kwa kubadilisha
tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa za mchezaji ili kufanikisha usajili
wao kwa msingi kwamba waligushi.
Uamuzi huu, ni wa mwisho na kwamba kama kuna
ambaye hajaridhika, ana nafasi ya kukata rufaa kwenye CAS - Mahakama ya
Mashauri ya Soka ya FIFA iliyoko Geneva, Uswisi.
Awali kwa nyakati tofauti, Pamba SC ya Mwanza na
The Mighty Elephant ya Songea zilikata rufaa kuilalamikia Abajalo FC kwa
kumtumia mchezaji wa Kaliua City ya Tabora, Laurence Mugia kutoka
Kagera Sugar katika michezo ya mtoano wa Ligi Daraja la Pili kwa ajili
ya kupanda daraja la kwanzaa huku wakijua kuwa ni kosa kwa mujibu wa
kanuni.
0 Comments