Blog ya Jamii na Michezo inaungana na wapenda michezo Tanzania pamoja na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa kutumia salamu za rambirambi kwa wanamichezo wote nchini na kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto kutokana na kifo cha Elizabeth Mayemba - Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Majira.
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa kutumia salamu za rambirambi kwa wanamichezo wote nchini na kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto kutokana na kifo cha Elizabeth Mayemba - Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Majira.
Rais Malinzi amesema, amepokea taarifa za kifo cha
mwandishi huyo mwandamizi wa habari za michezo nchini kilichotokea
Julai 09, 2016 na habari zake kuanza kusambaa majira ya jioni jana kabla
ya kuthibitishwa na wanafamilia na uongozi wa TASWA kupitia njia
mbalimbali za mawasiliano.
Salamu za rambirambi za Rais wa TFF Malinzi pia
zimekwenda kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka
kuwa na moyo wa subira wakati huu mgumu wa msiba wa Elizabeth Mayemba.
Elizabeth Mayemba, wakati wa uhai wake alikuwa na
mchango mkubwa katika tasnia ya habari za michezo akitoa mawazo yake
hivyo ameacha alama ya ucheshi, kujituma na uwajibikaji katika
kufanikisha kazi zake katika gazeti la Majira na wakati fulani magazeti
ya Kampuni ya New Habari House 2006.
Lakini pia uongozi
wa Kampuni ya Business Times Limited (BTL), inayozalisha Magazeti ya
Business Times, Majira na Spoti Starehe,alipokuwa anafanyafanyakazi Elizabeth Mayemba,imetoa taarifa juu ya misiba huo.
Elizabeth
Mayemba ambaye ni Kaimu Mhariri wa Michezo Gazeti la Majira alikutwa na
mauti Jumamosi ya Julai 9, 2016 saa 2 usiku, akiwa nyumbani kwake
Tabata Kisukulu, Dar es Salaam.
Kabla ya kukutwa na mauti, marehemu alifanya kazi zake na majukumu yote ya kila siku bila kuonesha dalili za kuumwa.
Akiwa nyumbani kwake saa 2 usiku, alijisikia vibaya na kukimbizwa hospitali ya Amana, akiwa njiani alikutwa na mauti.
Kwa
mujibu wa familia ya marehemu, Elizabeth Mayemba atazikwa siku ya
Jumanne ya Julai 12, 2016, mkoani Morogoro kwenye Makaburi ya Kola.
Elizabeth
Mayemba ataagwa Jumatatu ya Julai 11, 2016 saa 5.00 asubuhi nyumbani
kwake Tabata Kisukulu. Baada ya Misa mwili utasifirishwa kwenda Morogoro
kwa mazishi.
Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kila mara ili kuwapa nafasi watu wengi wajue ratiba zote zilivyopangwa.
Kampuni
imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na Elizabeth Mayemba, ambaye mchango
wake ulikuwa mkubwa zaidi na ulioonekana kwa kila mtu. Marehemu ameacha
mume na watoto watatu wa kiume.
Mungu Ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina
Meneja Mkuu
Business Times Limited
0 Comments