USIKU wa kuamkia leo kulifanyika tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2015/2016.
Tuzo hizo ambazo zilifanyika katika ukumbi wa Double Tree Hotel By Hilton, Masaki, Dar es Salaam.
kulikuwa na vipengele vingi,ambapo Aishi Salum Manula mchezaji wa Azam FC alinyakuwa tuzo ya kipa ambapo katika kipengere hicho alikua akishindana na Deo Munishi ‘Dida’ wa Yanga na Benno Kakolanya wa Prisons na kuzawadiwa Sh. Milioni 5.7
Mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara ni Amissi Tambwe wa Yanga akizawadiwa pia Sh. Milioni 5.7.
Thabani Michael Kamusoko ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Kigeni, akiwaangusha Mzimbabwe mwenzake anayecheza naye Yanga SC, Donald Ngoma na kipa Muivory Coast wa Simba, Vincent Agban hivyo kuzawadiwa Sh. Milioni 5.7 pia.
Kocha Mholanzi Hans van der Pluijm yeye ameshinda tuzo ya Kocha Bora huku akizawadiwa Sh. Milioni 8, ambapo katika kipengere hicho alikua akishindana na Mecky Maxime wa Mtibwa Sugar na Salum Mayanga wa Prisons.
Tshabalala ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi ambapo katika kipengere hicho alikua akishindana na Farid Mussa wa Azam na Shizza Kichuya wa Mtibwa Sugar na kuzawadiwa Sh. Milioni 4.
Ibrahim Hajib wa Simba ameshinda tuzo ya Bao Bora la Msimu na kuzawadiwa Sh. Milioni 3 akimshinda Tambwe wa Yanga ambaye alikuwa akichuana naye katika kipengere hicho.
Klabu ya Mtibwa Sugar imezibwaga JKT Ruvu na Mgambo Shooting katika tuzo ya Timu yenye Nidhamu na kuzawadiwa Sh. Milioni 17.2.
Klabu ya Mtibwa Sugar imezibwaga JKT Ruvu na Mgambo Shooting katika tuzo ya Timu yenye Nidhamu na kuzawadiwa Sh. Milioni 17.2.
Ngole Mwangole ameshinda tuzo ya Refa Bora na kuzawadiwa Sh. Milioni 5.7 ambapo katika kipengere hiko alikua akishindana na Anthony Kayombo na Rajab Mrope.
0 Comments