Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY 20,2016 SAA 11:49 JIONI
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), imeipiga faini ya Sh. 500,000, Klabu ya Namungo FC
ya
Lindi kwa kila mechi ambayo mchezaji Imani Vamwanga aliichezea timu
hiyo akitumia jina la Emmanuel T. Mwanga katika mashindano ya Ligi ya
Mabingwa wa Mikoa (RCL), kituo cha Morogoro 2015/2016.
Katika kikao kilichoketi Julai 14, 2016
kujadilina, kupitia, malalamiko na taarifa za waamuzi na Kamisaa za
mashindano ya RCL katika kituo cha Morogoro, kamati imebaini kwamba
Namungo ilifanya udanganyifu wa jina la mchezaji kwa kumsajili na
kumchezesha mchezaji Imani Vamwanga leseni Na. 930909003 ya usajili wa
Ligi Daraja la Kwanza FDL msimu wa 2015/2016 klabu ya Kurugenzi Mafinga
akitumia jina la Emmanuel T. Mwanga.
Kamati imebaini hayo kupitia taarifa za usajili,
ripoti za waamuzi na makamisaa kwa michezo ambayo mchezaji tajwa hapo
juu amecheza katika Mashindano ya Ligi ya mkoa wa Lindi na Mashindano ya
Ligi ya Daraja la Kwanza FDL msimu wa 2015/16. Namungo inaadhibiwa kwa
mujibu wa Kanuni ya 39 (1) inayozungumza adhabu kwa klabu.
Kamati ya Mashindano ya TFF imetoa uamuzi huo kwa
Namungo FC kupigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kila mechi ambayo mchezaji
Imani Vamwanga akitumia jina la Emmanuel T. Mwanga amecheza katika
mashindano ya RCL.
Pamoja na faini hiyo kwa kila mchezo ambao Namungo
ilimchezesha mcheza huyo, timu hiyo Kamati ya Mashindano ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeitangaza Namungo FC kupanda daraja
kwenda Ligi Daraja la pili msimu wa 2016/2017 kama ilivyoainishwa kwenye
kanuni ya 5 kipengere cha (4).
Kamati imejiridhisha kwa kupitia taarifa za
usajili, ripoti za waamuzi na makamisaa kwa michezo ambayo ilikuwa
inalalamikiwa imefikia uamuzi huo kwa mujibu wa kanuni za mashindano
hayo. Kamati imeipongeza na kukutakia kila la heri katika michezo.
Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kutoa pongezi zake za dhati kwa Klabu ya Pepsi FC ya Arusha kwa kupata nafasi ya kupanda daraja na kuingia Daraja la Pili SDL msimu wa 2016/2017.
Hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 5 kipengere cha (5) ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa RCL msimu wa 2015/2016.
Timu imefanikiwa kupata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya mabingwa wa Mikoa 2015/2016 kituo cha Singida na kuongoza kati ya timu zilizoshika nafasi ya pili katika vituo vilivyosalia ambavyo ni Njombe, Morogoro na Muleba. TFF inaItakia kila la kheri katika maandalizi ya kushiriki Daraja la Pili msimu wa 2016/2017.

0 Comments