Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17
(Serengeti Boys), kesho itaondoka nchini kuelekea nchini Madagascar kwa ajili
ya
kwenda kuendelea na kambi ya kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali
za Afrika kwa vijana dhidi ya Afrika kusini utakaochezwa mapema mwezi ujao.
Safari hiyo Sertengeti Boys ni ahadi iliyotolewa na rais wa
TFF Jamal Malinzi wakati timu hiyo ilipokua katika mchakato wa kucheza mchezo
wa awali wa kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Shelisheli, ambapo iliahidiwa
kwenda kuweka kambi nchini Madagascar kama wangeshinda mchezo huo, jambo ambalo
lilitimia.
Afisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF, Alfred Lucas
amesema maandalizi ya safari ya Serengeti Boys ambayo itakua na kituo Afrika
kusini yameshakamilika, na wana uhakika wa kambi ya nchini Madagascar itazaa
matunda ya kufanikisha ushindi.
Alfred Lucas amesema Wamemjumuisha golikipa wa zamani wa klabu ya Simba Juma Kaseja Ambaye ana class c ya ukocha katika benchi la ufundi akimsaidia kocha Bakari Shime katika unoaja wa makipa wa Serengeti Boys.
Pia Alfred Lucas amesema kikosi cha Vijana hao kitaondoka Bila ya kocha Msaidizi Sebastian Nkoma na Shilton ambao wanashiriki kozi ya Ukocha ya Fifa.
0 Comments