Ticker

6/recent/ticker-posts

UCHAGUZI YANGA SC UMEKAMILIKA,HAYA NDIYO MATOKEO RASMI

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 12,2016 SAA 07:24 MCHANA
Wajumbe waliochaguliwa(pich na Dick Dauda)
Mchakato mzima wa uchaguzi katika klabu ya Yanga Africans umemalizika salama na matokeo yamewekwa
hadharani.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro amesema Yusuph Manji ametangazwa mshindi baada kupata kura 1, 468 kati ya 1,470 zilizopigwa huku kura mbili tu zikiharibika na hakukuwa na hakukua na mpinzani katika nafasi hiyo.

Makamu Mwenyekiti ni Clement Sanga ameibuka mshindi baada ya kujizolea kura 1, 428 kati ya 1,508 zilizopigwa, huku mpinzani wake,Titus Osoro akiambulia kura 80 tu.

Wajumbe waliochaguliwa

Nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Siza Augustino Lymo kura 1027, Omary Said Amir kura 1069, Tobias Lingalangala kura 889, Salum Mkemi kura 894, Ayoub Nyenzi kura 889, Samuel Lukumay kura 818, Hashim Abdallah kura 727 na Hussein Nyika kura 770.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Yanga Sam Mapande (katikati) akitangaza matokeo ya uchaguzi mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kuhesabu kura


Idadi ya wajumbe 12 wameshindwa kuibuka na ushindi baada ya kura kuwa pungufu ambao ni David Luhago kura 582, Godfrey Mheluka kura 430, Ramadhani Kampira kura 182, Edgar Chibura kura 72, Mchafu Chakoma kura 69, George Manyama kura 249, Bakari Malima kura 577, Lameck Nyambaya kura 655, Beda Tindwa kura 452, Athumani Kihamia kura 558, Pascal Lizer kura 178 na Silvester Haule kura 197.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments