Kikosi cha cha kwanza cha timu ya taifa ya vijana ya Tanzaia chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoifunga 3-0 Shelisheli |
Timu ya
taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys),Usiku wa kuamkia leo inatarajia
kuondoka nchini kuelekea visiwani Shelisheli
tayari kwa mchezo wa mkondo wa
pili wa kuwani nafasi ya kushiriki fainali za Afrika kwa vijana zitakazofanyika
nchini Madagascar mwaka 2017.
Kocha mkuu
Bakari Shime ameteua kikosi cha wachezaji 20 ambao watasafiri na timu hiyo
kesho kuelekea visiwani Shelisheli, huku akiwaachama wachezaji wengine wane ambao
wanakabiliwa na majeraha.
Kikosi cha kwanza cha Shelisheli kilichofungwa na
Serengeti Boys 3-0 |
Maandalizi ya safari kwa Serengeti Boys yameshakamilika
baada ya kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri katika mchezo wa mkondo
wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam, mwishoni mwa juma lililopita.
Benchi la ufundi la Serengeti Boys |
Kocha mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime amesema kikosi chake kipo tayari
kwa safari pamoja na mpambano huo wa mwishoni mwa juma hili.
Amesema amekiandaa
kikosi chake kwa ajili ya kupata ushindi popote pale, hivyo hana shaka na
maandalizi aliyoyafanya kabl ya kupambana na Shelisheli katika mchezo wa mkondo
wa pili.
0 Comments