Mabao yote ya Misri yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea ya England, Mohammed Salah dakika ya 43 kipindi cha kwanza kwa shuti la mpira wa adhabu baada ya beki Mwinyi Hajji Mngwali kumkwatua nje kidogo ya boksi Nagram Fahmy.
Salah akaifungia bao lake la pili kwa Misri dakika ya 58 baada ya kumpita beki wa kushoto, Mwinyi Hajji Mngwali.
Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta alikosa penalti baada ya Himid Mao kuangushwa ndani ya enero la hatari.
Mchezo huo ulikuwa ni mchezo wa tatu kwa Taifa Stars, lakini ulikuwa ni mchezo wa marudiano na timu ya taifa ya Misri baada ya mchezo wa kwanza kuchezwa Misri June 14 2015 katika mji wa Alexandria na kumalizika kwa Taifa Stars kufungwa jumla ya magoli 3-0.
Taifa Stars sasa wametolewa rasmi katika michuano ya kuwania kufuzu AFCON 2017, lakini imebaki na mchezo mmoja wa kukamilisha ratiba itakayocheza September mwaka huu dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria (Super Eagles), Misri imefikisha jumla ya point 10, Taifa Stars point moja na Nigeria ina point 2.
ANGALIA PICHA
Kikosi cha Tanzania; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali/Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ dk68, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Himid Mao, Thomas Ulimwengu/Deus Kaseke dk73, Mwinyi Kazimoto, Elias Maguli/John Bocco dk62, Mbwana Samatta na Farid Mussa.
Kikosi cha Misri; Essam Kamal Tawfik, Alg Gabr Mossad, Ramy Hisham Abdel, Mohamed Abdel Sayed, Abood Abdulrahamn Amed, Tarek Hamad Hamed, Mohamed Nasser Elsayed, Mohamem Ahmed Ibrahim/Amr Medhat dk63, Abdallah Mahamoud Said na Nagram Mohsin Fahmy.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .





















0 Comments