Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:NI KWELI AMIS TAMBWE NA DONALD NGOMA WAMEPIGANA UTURUKI ? Jerry Muro amejibu swali hilo...


 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 25,2016 SAA 10:34 JIONI

Baadhi ya wachezaji wa klabu bingwa Tanzania bara Young Africans, hii leo wamewasili nchini tayari kwa kuendelea na
maandalizi ya mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho la soka barani Afrika CAF dhidi ya TP Mazembe uliopangwa kuchezwa siku ya jumanne kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa klabu ya Young Africans, Jerry Muro amesema kundi linguine la wachezaji lilitarajiwa kuwasili jijini humo majira ya jioni likitokea mjini Antalia nchini Uturuki walipokua wameweka kambi ya kujiandaa na mchezo huo.

Muro pia amezungumzia maandali ya mchezo huo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi nchini, kutokana na uzito wa klabu ya TP Mazembe katika ukanda wa Bara la Afrika ambao mwaka jana walitwaa ubingwa wa bara hilo.

SIKILIZA HAPA
JKuhusu taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii juu ya ugomvi unaodaiwa kutokea katika kambi ya nchini Uturuki kati ya washambuliaji Amis Tambwe na Donald Ngoma, Jerry Muro amesema taarifa hizo sio za kweli na zimekua zikizishwa kwa makusudi ya kutaka kuwaondoa wachezaji wao kwenye fikra za kimchezo.

Hata hivyo katika mkutano huo, suala la mpangilio wa mashabiki kwenye uwanja wa taifa ambalo limekua likisisitizwa na shirikisho la soka nchini TFF likajitokeza, ambapo Jerry Muro ameendelea kupingana nalo huku akitolea mfano wa namna wanavyokutana na mazingira tofauti katika viwanja vingine wanapokwenda kucheza michezo yao ya ugenini.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments