Ticker

6/recent/ticker-posts

WAAMUZI WA YANGA WAWEKWA HADHARANI

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.May.5,2016 SAA 12:59 JIONI

Mwamuzi Joseph Odartei Lamptey, Jumamosi Mei 7, 2016 anatarajiwa kuwa mwamzi wa kati katika mchezo wa
kimataifa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaozikutanisha timu za Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na GD Sagrada Esperanca ya Angola.
Lamptey kutoka jiji la Accra, Ghana atasaidiwa na raia wenzake wa nchi hiyo kuchezesha mchezo huo Na. 99. Mwamuzi Msaidizi Na. 1 (line 1) ni David Laryea wakati Mwamuzi Msaidizi Na. 2 (line 2) ni Malik Alidu Salifu.
Mwamuzi Msaidizi mezani (Fourth Official) ni Cecil Amately Fleischer huku Kamishna wa mchezo huo, akiwa ni Asfaw Luleseged Begashaw wa Ethiopia.
Viingilio na upatikanaji wa tiketi utatangazwa kesho Ijumaa Mei 6, 2016 na uongozi wa klabu ya Young African mara baada ya mkutano kati ya makocha wa timu zote mbili. Mkutano wa makocha hao utafanyika saa 5.00 mchana kwenye Ukumbi wa mikutano wa TFF.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments