Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.May.28,2016 SAA 08:30 MCHANA
Msimu mpya wa kipindi cha Maisha Plus umezinduliwa hapo jana usiku katika viwanja vya Studio za Azam Tv ambapo
kauli mbiu ya mwaka huu ni HAPA KAZI TU.
Kipindi cha Maisha Plus Kilianza Rasmi mwaka 2008 mwishoni kikiwa na lengo la kuwawezesha vijana kuwa na uwezo wa kufikiri,ujasiri na kuwafanya vijana kuweza kupambana katika kutafuta maisha ya uhalali.
Katika msimu wa kwanza ambao ulichukuwa vijana kutuka mikoa 8 nchini Tanzania na Mshindi aliyekuwa Abdul alijishindia milioni 10,msimu wa pili mwaka 2009 uliohusisha mikoa 13 mshindi ambaye alikuwa ni Alex Mabinza aliondoka na milioni 15,Msimu wa Tatu ambao ulitanuwa wigo kwa mikoa kadhaa ya Tanzania lakini pia ulivuka mipaka kwa kuhusisha nchi ya Kenya,Burundi,Rwanda na Uganda na mshindi mwanadada Bereniki Kimoro akatokea Tanzania akachukuwa milioni 20.Msimu wa 4 pia Zawadi iliongezeka tena ikawa milioni 25 alizozichuwa Boniface.
Katika Msimu Mpya wa Maisha Plus utakaoanza kesho kwa kuoneshwa na Kituo cha Azam Two majira ya Saa Tatu Usiku mshindi atajijishindia Shilingi Milioni 30,ambapo Mkurugenzi wa Azam Media, Tido Mhando alisema kuwa wamejipanga kutoa burudani ya tofauti ambapo utakuwa na nchi kama Burundi, Rwanda na nyinginezo ambazo ni majirani zetu na zote hizo zitatoa washiriki wanne kila moja hivyo kwa nchi za jirani kutakuwa na washiriki 16 na hapa Tanzania kutakuwa na washiriki 14 jumla watakuwa 30.
ANGALIA PICHA
ANGALIA PICHA
![]() |
| Muanzilishi wa Maisha Plus, Masoud Kipanya akifungua rasmi sherehe za uzinduzi huo. |
![]() |
| Baadhi ya wageni waalikwa waliofika jana katika uzinduzi wa maisha plus wakifuatilia kwa makini |
![]() |
| Wasanii Jhikoman na Vitali Maembe wakitoa burudani katika uzinduzi huo. |
![]() |
| Aliyekuwa mshindi wa kwanza wa Maisha Plus Abdul akizungumza katika uzinduzi huo. |
![]() |
| Masoud Kipanya akimpa nafasi ya kuongea mshindi wa msimu wa pili wa Maisha Plus, Bernick Kimiro. |
![]() |
| Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza (katikati) ndiye ailizindua msimu mpya wa Maisha Plus Siku ya Jana. |
![]() |
| Baadhi ya Washikiri wa maisha Plus wa misimu tofauti wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Azam Media Tido Mhando (kulia) |











0 Comments