Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:MSIKILIZE JERRY MURO AKIWAOMBA RADHI SIMBA SC

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.May.19,2016 SAA 08:39 USIKU

Uongozi wa klabu ya Young Africans umetoa shukurani kwa wanachama pamoja na mashabiki wa klabu hiyo, kufuatia hatua ya
kuwa pamoja na kikosi chao tangu kilipoanza kampeni ya kushiriki michuano ya kimataifa kwa mwaka 2016.

Mashabiki na wanachama wa Young Africans wamepewa shukurani hizo, kufuatia mafanikio ya kikosi chao ya kutinga katika hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho la soka barani Afrika, baada ya kupata ushidni wa jumla wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Sagrada Esperanca ya nchini Angola.

Mbali na shukurani kwa mashabiki na wanachama zilizotolewa na uongozi wa Young Africans, kupitia idara ya habari na mawasilino inayoongozwa na Jerry Muro, pia wawakilishi hao pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa wameshusha lawama kwa mwamuzi aliyechezesha mchezo wa jana kwa kumtuhumu kuwa chanzo cha mapungufu yaliyojitokeza.


Kuhusu kuwasili kwa kikosi cha Young Africans, Muro amesema mashujaa wao wameshafika nchini Afrika kusini kwa lengo la kusubiri usafiri wa ndege, na kinatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam kesho mishale ya mchana.

Katika hatua nyingine Muro, amelitaka shirikisho la soka nchini TFF kufikiria mara mbili kuhusu mabadiliko ya tarehe ya mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la shirikisho la soka ambao umerejeshwa nyuma na sasa utachezwa May 25 badala ya Juni 11.

Wakati huo huo huo Jerry Muro, ametumia nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari, kupenyeza ujumbe kwa mahasimu wao Simba, kwa kuwataka radhi kufutia maneno makali aliyokua akiyazungumza wakati wote wa msimu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara ambao utafikia kikomo mwishoni mwa juma hili.


SIKILIZA HAPA

K

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .


Post a Comment

0 Comments