Kundi kubwa la mashabiki wa klabu ya Young Africans, Ijumaa ya tarehe 20 May 2016 lilifika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Mwalimu Nyerere, kwa ajili ya kukikopokea kikosi chao kikitokea nchini Angola kupitia Afrika kusini.
Mwalimu Nyerere, kwa ajili ya kukikopokea kikosi chao kikitokea nchini Angola kupitia Afrika kusini.
![]() |
| Mlinda mlango Deogratius Munish Dida akizungumza katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere |
Mashabiki wa Young Africans walifika uwanjani hapo wakiwa na furaha, Nderemo na Bashasha kufuatia kikosi chao kufanikisha azma ya kusonga mbele kwenye michuano ya kombe la shirikisho, licha ya kufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya G.D. Sagrada Esperança.
Mlinda mlango Deogratius Munish Dida, alionekana kuwa shujaa miongoni mwa wachezaji wa Young Africans walikua wakiwasili uwanjani hapo, kufutia kitendo cha wanachama na mashabiki kumshabikia kwa kumuimbia nyimbo za kumpongeza kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha katika mchezo wa jusi dhidi ya G.D. Sagrada Esperança.
MSIKILIZE DEOGRATIUS MUNISH DIDA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI




0 Comments