Klabu ya Simba hii leo imewasirisha barua katika shirikikisho la soka nchini Tanzania Tff kueleza Msimamo wao kuwa
hawatacheza mechi ya Ligi kuu kama hakutakuwa na marekebisho ya ratiba,pia Kama baadhi ya timu za ligi hiyo hazita kamilisha viporo vyao.
Simba imeitaka bodi ya ligi kufanya mabadiliko ya ratiba.
Klabu ya Simba imekuwa ikilalamikia viporo kwa baadhi ya timu wakisema kuwa kunatengenezwa mazingira ya kupata matokeo ya ubingwa kwa timu hizo.
Katika barua hiyo pia Simba wameiandikia Tff kuhusu marejeo ya hukumu ya Ramadhani Singano (Messi) waliyoitoa kamati ya hadhi na wachezaji.
Simba wamemperekea barua hiyo kwa Waziri mwenye dhamana ya Michezo Nape Nnauye ili ajue kinachoendelea.
katika hatua nyingine Simba imezungumzia Swala la mcchezaji wao Abdi Banda, Simba wamemuandikia barua mchezaji huyo ili ajue makosa yake na baada ya hapo kamati ya utendaji itakutani kwa ajili ya kutoa maamuzi.
Banda ameripotiwa na klabu hiyo kufanya makosa kadhaa ya kinidhamu.

0 Comments