Baada ya kulalamika kupitia vyombo vya habari huku wakidai waliwahi kuwaandikia barua TFF kuhusu kuvurugwa kwa ratiba ya ligi kuu ya soka
Tanzania bara msimu wa 2015-16, wekundu wa Msimbazi Simba wameibuka na kudai malalamiko hayo wanayahamishia ofisini kwa waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa Na Michezo Nape Nnauye.
Simba wamefikia hatua hiyo baada ya kuona wanaendelea kucheza michezo yao kama kawaida huku wapinzani wao katika mbio za ubingwa wakibaki nyuma kwa tofauti ya michezo miwli hadi mitatu, hali ambayo wanaamini itavuruga mikakati yao ya kumaliza kiu ya ubingwa uliyodumu Msimbazi kwa zaidi ya miaka minne.
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema wanaamini malalamiko yao wakiyafikisha katoka ofisi ya waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa Na Michezo Nape Nnauye huenda yakasikilizwa na kufanyiwa upembuzi yakinifu kabla ya kupatiwa majibu sahihi.
Lakini pia Haji Manara ameendelea kuwakumbusha TFF kutimiza ahadia mbazo waliwahi kuzitoa mbele ya vyombi vya habari, kuhusu utovu wa nidhamua mbao uliwahi kuonyesha dhidi yao.
katika hatua nyingine Uongozi wa klabu ya Simba umempunguzia adhabu beki wake Hassan Isihaka, ambaye alifungiwa kwa muda usiojulikana kufuatia utovu wa nidhamu aliouonyesha dhidi ya kocha Jackson Mayanga kabla ya mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Singida United.
Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara, amesema kwa sasa beki huyo ataendelea kulipwa nusu mshahara hadi atakaporejea huku wakimvua wadhifa mkubwa aliokua nao kikosini.
Wakati huo huo kocha wa kikosi cha Simba Jackson Mayanja amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri kuelekea katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Coastal Union ambao utachezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.
Mayanja amesema kikosi chake kitakwenda jijini Tanga kucheza soka la kushambulia kama inavyokua katika michezo ya nyumbani, ili kutimiza wajibu wa kumaliza utata wa kupata point tatu kwenye uwanja wa Mkwakwani.
Amesema wachezaji wote wapo katika hali nzuri, na waliokua majeruhi wamenza kurejea katika mipango yake taratibu taratibu.
Katika hatua nyingine wakuu wa matawi ya klabu ya Simba, hii leo wamekutana kwa lengo la kupanga mikakati ya mchezo huo wa siku ya jumamosi ambao unatazamiwa kuwa na vuta nikuvute.
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu ya Simba Idd Kajuna, alikua sehemu ya kikosi hicho na alipewa jukumu la kusema mikakati waliyokubaliana mbele ya waandishi wa habari.

0 Comments