Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika, Young Africans wamejinasibu kuwa tayari na
mpambano wa mkondo wa pili dhidi ya mabingwa wa soka kutoka nchini rwanda APR utakaochezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa klabu ya Young Africans, Jerry Muro hii leo alizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam na kueleza mipango mikakati ya kuelekea katika pambano hilo pamoja namaandalizi yake.
Muro amesema maandalizi kwa ujumla yamekaa vyama huku wakiamini mashabiki wa Young Africans pamoja na wengine wataelekea kuwanjani kwa wingi kutokana na viingilio walivyovipanga.
Katika hatua nyingine Jerry Muro amesema klabu ya Young African haina nia mbaya ya kuzuia vituo vya televisheni kuuonyesha moja kwa moja mchezo wao na APR, zaidi ya kutaka utaratibu wa mzungumzo kufanywa ili kila jambo liwekwe sawa.
Amesema haki za matangazo ya televisheni ya mchezo huo zipo mikononi mwao hivyo ni jukumu la kituo kinachohitaji kuonyesha mchezo huo kuwafuata na kuweka ofa mezani.

0 Comments