Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
Jumamosi kati ya watani wa jadi Simba SC dhidi ya Yanga SC utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku kiingilio cha chini kikiwa ni Shilingi elfu saba tu (7,000).
Kiingilio cha juu cha mchezo huo kitakua shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, Elfu Ishirini (20,000) VIP B & C, Elfu Kumi (10,000) kwa viti vya rangi ya machungwa (Orange), na Elfu Saba (7,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.
Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa saa 2 kamili asubuhi katika vituo vya TFF (Karume), Buguruni Olicom, Ubungo Oilcom, Kidongo Chekundu (Mnazi Mmoja), Posta (Agip), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Taifa, Makumbusho Stand, Kivukoni Ferry.
Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi wote wenye beji za FIFA, mwamuzi wa katikati Jonesia Rukyaa (Kagera), akisaidiwa na Josephat Bulali (Tanga), Samwel Mpenzu (Arusha), mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) huku Kamisaa wa mchezo huo akiwa Khalid Bitebo (Mwanza).
Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea Jumamosi kwa michezo sita, Young Africans v Simba (Taifa), Mbeya City v Azam (Sokoine), Stand United v JKT Ruvu (Kambarage), Toto Africans v Kagera Sugar (CCM Kirumba), Mgambo Shooting v Tanzania Prisons (Mkwakwani) na Majimaji FC v Mtibwa Sugar (Majimaji).
Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa michezo miwili, Mwadui FC v Coastal Union uwanja wa Mwadui Complex, huku Ndanda FC wakicheza dhidi ya African Sports uwanja wa Nagwanda Sijaon mjini Mtwara.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments