Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes League) inatarajiwa kumalizika wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa kwa wakati
mmoja katika viwanja mbalimbali nchini, huku Kundi A na C zikisaka vinara watakaopnda Ligi Kuu msimu ujao.
Bodi ya Ligi (TPLB) imeviandikia barua vilabu vyote vinavyoshiriki Ligi hiyo, wasimamizi wa vituo kuwafahamisha kuwa mechi zote zinatakiwa kuchezwa kwa muda mmoja na kusisitiza kuwa mechi zote zitaanza saa 10 kamili jioni bila kujali kama jua linawahi au kuchelewa kuzama.
Ni jukumu la Msimamizi na Kamishna kuhakikisha mechi yake inaanza katika muda uliotajwa (saa 10 kamili) bila kukosa. Utekelezaji wa maelekezo haya ni muhimu ikiwa ni moja ya njia ya kukabiliana na vitendo vyovyote vya upangaji wa matokeo vinavyoweza kujitokeza.
Mechi za mwisho za Kundi A hatua ya kwanza ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Friends Rangers FC vs Kiluvya United FC (Mabatini), Polisi Dar vs Polisi Dodoma (Shirika la Elimu Kibaha), Ashanti United vs African Lyon (Karume) na Mji Mkuu vs Kinondoni Municipal Council FC zitachezwa Februari 14, 2016 katika viwanja husika.
Mechi za mwisho za Kundi B hatua ya kwanza ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Kimondo Super SC vs Kurugenzi FC (Vwawa), Njombe Mji vs Lipuli FC (Amani), Ruvu Shooting vs Polisi Morogoro (Mabatini) na Burkina FC vs JKT Mlale (Jamhuri) zitachezwa Februari 13, 2016.
Mechi za mwisho za Kundi C hatua ya kwanza ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Mbao FC vs Polisi Mara (CCM Kirumba), Polisi Tabora vs JKT Oljoro (Ali Hassani Mwinyi) na JKT Kanembwa vs Geita Gold (Lake Tanganyika) zitachezwa Februari 13, 2016 katika viwanja husika.
LIGI DARAJA LA PILI KUENDELEA WIKIENDI
Ligi Daraja la Pili (SDL) nchini inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu zote 24 kucheza katika viwanja mbalimbali, kusaka timu nne za juu kutoka kila kundi zitazokpanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Jumapili Kundi A, Mvuvumwa FC watawakaribisha Singida United katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Mirambo FC watacheza dhidi ya Green Warriors uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, huku siku ya jumatatu Abajalo Tabora wakichuana dhidi ya Transit Camp katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Kundi B, Jumapili Pamba FC watacheza dhidi ya Alliance Schools uwanja wa CCM Kirumba, JKT Rwamkoma watawakaribisha AFC ya Arusha kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma, huku siku ya Jumatatu Bulyanhulu FC wakicheza dhidi ya Madini FC kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Kundi C, Jumatatu Mshikamano watawakaribisha Cosmopolitan uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, Karikaoo FC watawakaribisha Villa Squad uwanja wa Ilulu mjini Lindi, huku Changanyikeni wakicheza dhidi ya Abajalo Dar kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Kundi D, Kesho Jumamosi African Wanderes watawakaribisha The Mighty Elephant uwanja wa Wambi Mafinga, Jumapili Mkamba Rangers watacheza dhidi ya Sabasaba, huku Wenda FC wakicheza dhidi ya Mbeya Warriors katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments