Mabingwa wa soka Tanzania bara, Dar es salaam Young Africans wameahirisha safari ya kuelekea nchini Mauritius,
kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Cercle de Joachim.
kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Cercle de Joachim.
Kikosi cha Dar es salaam Young Africans kilitarajiwa kusafiri mapema siku ya jumatano kuelekea nchini Mauritius kwa usafiri wa ndege ya abiria, lakini sababu za maamuzi ambayo yamefikiwa na viongozi wa klabu hiyo kongwe hapa nchini yameafiki kikosi kuondoka siku moja kabla ya mchezo.
Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa Dar es salaam Young Africans, Jerry Murro amesema wameona kuna umuhimu wa kubadili mfumo wa safari yao ya kuelelekea nchini Mauritius, baada ya kujiridhidha na taarifa za kiiteligensia ambazo wamekua wakizipokea kutoka kwa wadau na mashabiki wao.
MSIKILIZE JERRY MURRO AKITOA SABABU
Hata hivyo Jerry Murro, ametoa ufafanuzi wa kina juu ya taarifa kiitelijensia ambazo anadai wamezipokea kutoka kwa wadau na wanachama wa klabu ya Dar es salaam Young African kutoka Afrika kusini pamoja na Mauritius, kwa kusema huenda kungejitokeza figisu figisu endapo kikosi chao kingeondoka hii leo.
Amesema baadhi ya taratibu za safari yao ya hii leo Jumatano ambayo wameiahirisha zilikua zinaviashiria vya kufanyika kwa mipango ya nje ya uwanja dhidi ya kikosi cha Dar es salaam Young Africans ambacho kwa msimu huu kimedhamiria kupambana na kufikia malengo ya kucheza hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments