Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.OCTO.17,2015 SAA 02:50 USIKU
Mheshimiwa Rais Jakaya M. Kikwete, Rais wa Jamhuri wa Tanzania mbele ya umati wa watu elfu moja amefungua
rasmi kituo kipya cha vijana; kilichopewa jina lake mwenyewe kama heshima kwake.
Maofisa Waandamizi kutoka kampuni ya Symbion Power, Timu ya Soka ya Sunderland inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza na Shirikisho la Mpira wa Kikapu la nchini Marekani wameungana na Mhe. Rais katika shughuli hii iliyoonyesha heshima kubwa kwa Vijana wa Dar es Salaam.
Tukio hili lilifanyika nyakati za Alasiri lilihusisha utumbuizaji kutoka kwa kikosi cha Timu ya Mpira wa Kikapu kiitwacho Atlanta Hawks Sky na Mchezaji wa zamani wa Timu ya Soka ya Sunderland, Kevin Ball.
Aidha tukio hili lilihusisha makocha wenye taaluma ya ukocha wa Mpira wa Miguu na Mpira wa Kikapu kusaidia kuboresha ujuzi wa Vijana wa Kitanzania.
Kituo kitakuwa wazi kwa siku zote saba za wiki kwa mwaka mzima kuanzia tarehe 19 Oktoba.
Mhe. Rais Kikwete alisema “Kitu muhimu ni kukuza vipaji vingali vichanga. Unatambua kipaji. Unakikuza.Hatukuwahi kuwa na kituo kama hiki. Na hiki kitakuwa ni cha namna ya kipekee. Kwangu mimi naona kuna hamasa kubwa kuhusu hiki kituo’’
Symbion, kituo kikubwa binafsi cha Kimarekani kinachozalisha umeme kina mahusiano ya karibu na Tanzania kupitia miradi ya umeme mbalimbali iliyoko nchini; kimesaidia ufadhili wa Kituo. Mkurugenzi Mkuu wa Symbion, Ndugu Paul Hinks anasema “ Hii ni kazi kubwa ya upendo sio tu kwa Symbion pekee bali pia kwa Timu ya Soka ya Sunderland na Shirikisho la Mpira wa Kikapu (NBA).
Kinachofanya hiki kitu kuwa cha kipekee ni kwamba hayo Mashirika mawili yanatoa msaada wa mafunzo ili kuweza kukuza wachezaji wa kiwango kizuri kwa wale wanaofika kwenye kituo hiki, kufikia vile viwango vya Wachezaji walioko kwenye shule za Mpira wa miguu na Mpira wa kikapu huko nje ya nchi. Matokeo ya Mafunzo haya yatakuwa ni uwepo wa kiwango kizuri cha Michezo kutoka Tanzania”
Kituo kitakuwa na kiwanja kikubwa aina ya 3G chenye nyasi bandia, viwanja viwili vinavyoruhusu wachezaji kucheza watano watano kila upande, Kiwanja kimoja cha Mchanga, Viwanja viwili vya mpira wa kikapu pamoja na taa za mwanga mkali ili kuwezesha Wanajamii kufurahia huduma za hiki kituo nyakati za jioni.
Mshirika wa Kituo cha JMK, Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Marekani (NBA) ataendesha ligi ya Mpira wa kikapu kwa vijana maarufu kama Jr. NBA League nchini Tanzania; Itakayohusisha timu 30 kutoka shule mbalimbali jijini Dar es Salaam. Ligi hii italeta kwa ukaribu hamasa ya Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA) na hivi kuwahamasisha wavulana na wasichana kwa wingi zaidi kushiriki katika mchezo wa mpira wa kikapu kwa kupitia njia nzuri inayofurahisha na uzoefu chanya vipatikanavyo kwenye mchezo huu. Ligi hii pia inaleta sifa kubwa kwenye maisha kama Kufanya kazi kwa pamoja, uongozi, ukakamavu na namna nzuri ya kuishi kwa kushiriki kwenye michezo na mashindano.
Timu ya Soka ya Sunderland itatoa msaada wa mafunzo na mazoezi katika kukuza huu mradi; ambapo maelfu ya vijana watafaidika kwa kufanya kwa pamoja michezo, elimu na ushiriki wa Wananchi kupata ujuzi na utaalam kutoka kwa Timu ya Soka ya Sunderland na shule yake ya Michezo ambayo imefanikiwa kwa kiwango cha juu.
Vile vile wakati wa Uzinduzi Margaret Byrne, Mkurugenzi Mkuu wa Sunderland alisema “ Mchezo wa Mpira wa miguu kwenye Jamii ulikuwa ndio mwanzo wa Wachezaji wetu wengi. Unatoa muundo bora wa kukua na kuendelea sio kuwa mchezaji tu bali na kuwa Mtu mwenye nidhamu. Unafundisha ubora wa uongozi, uwajibikaji, uvumilivu na kufanya kazi kwa pamoja’’
Aidha Mama huyu aliongeza “ Huduma katika kituo cha vijana cha Michezo vinadhihirisha kiu ya Timu ya Soka ya Sunderland kwa umma unaozunguka eneo inapofanyia kazi na utasaidia kizazi kipya na Wachezaji nyota wa Kitanzania na hivi kutoa fursa muafaka kabisa kwa vijana wa Dar es Salaam kulea vipaji vyao na kujiendeleza zaidi”
Kituo kitakuwa na kitengo cha ubora uliotukuka kitakachokuwa na jukumu la kuboresha stadi za Wachezaji wadogo wanaocheza mpira wa miguu. Hiki kitengo kitaanza kufanya kazi rasimi Januari 2016 na kitakuwa na progamu iliyobuniwa na Timu ya Soka ya Sunderland.
Grassroot Soccer, ambayo lengo lake ni kutumia michezo kuelimisha, kuhamasisha na kuleta vijana pamoja waishi maisha mazuri itahusika kama mshiriki katika kuweka mipango mbalimbali ya kituo.
Baada ya kushuhudia vijana wa kitanzania wakijifunza kuhusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI kuptia mpira wa miguu wakati wa shughuli za uzinduzi wa kituo, Meneja Ubia wa GRS Mama Sarah Miller alisema “ Vijana wanapowezeshwa, wanaweza kubadili Ulimwengu. Wanapopewa nafasi ya kukua, sikio sikivu lililotayari kusikiliza na nguvu ya msaada wa mara kwa mara; vijana watajenga Ulimwengu wa kizazi kijacho, Tunaamini kwamba leo imekuwa ni hatua mojawapo katika kufanikisha lengo la
kuwawezesha vijana kuishi maisha yanazingatia afya Tanzania nzima”
Kituo kitafunguliwa rasmi kwa umma tarehe 19 Oktoba lakini ili kuweza kutumia huduma zinazopatikana hapa; itampasa mhitaji kusajili maelezo binafsi mafupi. Wananchi wanaweza kujaza fomu ya kujisajili kwa kutumia njia tofauti. Kwa kuja kwenye eneo la kituo; au kwa kutuma barua pepe kupitia info@jmkpark.org na kuomba fomu ya kujisajili. Mara fomu itakapokuwa imekamilika kujazwa, waweza kuituma kwa njia ya barua pepe kupitia info@jmkpark.org au kuileta kwa mkono na kuicha kwenye nyumba ya mlinzi pale kwenye lango kuu lililoko mtaa wa Makamba mkabala na Hekalu la Singa Singa ( Sikh Temple).
Kwa habari mpya mpya kuhusu kituo tafadhali wasiliana nasi kupitia akaunti yetu ya Twitter @jmkpark na Instagram @jmk_park
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments