Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.OCTO.23,2015 SAA 01:40 USIKU
Timu ya taifa ya mpira wa magongo (Hockey) ya wanawake kesho inacheza mechi yake ya kwanza ya ufunguzi dhidi ya
Zimbambwe itakayopigwa nchini Afrika kusini,katika mashindano kuwania kufuzu michuano ya Olympic ya mwaka 2016 ambayo itafanyika mjini Rio de Janeiro, nchini Brazil.
Zimbambwe itakayopigwa nchini Afrika kusini,katika mashindano kuwania kufuzu michuano ya Olympic ya mwaka 2016 ambayo itafanyika mjini Rio de Janeiro, nchini Brazil.
Kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya mpira wa Magongo Varentina Quaranta amesema kwa upande wa wanaume mechi yao ya ufunguzi watacheza na Misri siku ya jumapili.
Kocha Quaranta ambaye yuko na timu nchini afrika kusini amesema wachezaji wote wako tayari na morali ya kutosha kuelekea katika mashindano hayo,huku pia akitoa shukrani kwa benki ya NMB na baadhi ya wadau wa mchezo huo kwa kuwezesha safari hiyo
MSIKILIZE ZAIDI VARENTINA QUARANTA
"TIMU ZOTE MBILI ZIMEFIKA SALAMA SIKU YA JUMATATU NA TUMECHUKUA SIKU HIZI TATU KWA KUZOEA HALI YA HEWA HAPA, PAMOJA NA CHAKULA NA ACCOMODATION. TUMEFANYA MAZOEZI KATIKA UWANJA WA ASTROTUF YA RANDBURG HOCKEY STADIUM (JOHANESBURG) MARA TATU NA TUMECHEZA METCHI MBILI YA KIRAFIKI. KESHO TUNAFUNGUA MASHINDANO NA METCHI YETU AGAINST ZIMBABWE WANAWAKE SAA NANE NA NUSU MCHANA, HALAFU TUTACHEZA TENA JUMATATU TAREHE 26 NA KENYA, TAREHE 28 NA NAGERIA, TAREHE 29 NA GHANA, TAREHE 31 NA SOUTH AFRICA NA TAREHE 1 MWEZI WA TISA NA NAMIBIA."Amesema Varentina Quaranta
"MASHINDANO YATAKUWA NGUMU. KWA UPANDE WA WANAUME, WATAANZA MASHINDANO JUMAPILI TAREHE 25 NA EGYPT, COACH NICK ISBOUTS NA MSAIDIZI WAKE MERICA KAHOLA, WANAFANYA NAO MAZOEZI KILA SIKU KUJINDAA VIZURI NA KUKAMILISHA TIMU ILI IWE TAYARI KUSHIDANA NA TIMU YA EGYPT JUMAPILI."
"TIMU ZOTE MBILI ZIKO VIZURI, WACHEZAJI WANAJITAHIDI KUSHINDANA NA TIMU ZINGINE KADRI WANAOWEZA, KINACHOTUCOSTI NI KUTOKUWA TUMEZOEA KUCHEZA NA UWANJA WA ASTROTURF KAMA TIMU ZINGINE, NA PIA EXPERIENCE YA WACHEZAJI WETU NI NDOGO KULINGANA NA TIMU ZINGINE."
"LAKINI TUTAJITAHIDI, NA PIA TUNATAKA KUWASHUKURU TENA WADHAMINI WETU WA NMB, KWA KUTUWEZSHA KUJA HAPA SOUTH AFRICA NA TUTAWAADHI KWAMBA TUTAJITAHIDI KUPATA MATOKEAO MAZURI."amefafanua kocha Varentina Quaranta
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments