Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, hii leo imesaini mkataba wa miaka mitatu ya kudhamini ligi kuu soka Tanzania
bara baada ya kufikia makubaliano na Shirikisho la soka nchini TFF kupitia Bodi ya ligi.
Sehemu ya mkataba huo inaeleza kiasi cha shilingi za Kitanzania Bilioni 1.2 kinakwenda moja kwa moja kwenye klabu 16 ambazo zitapapatuana kwa ajili ya kuuwani ubingwa wa Tanzania bara msimu wa 2015-16.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom Tanzanaa Kelvin Twissa, amesema hatua ya kutiliana saini na TFF kupitia bodi ya ligi, inaendelea kudhihirisha uhusiano mzuri uliopo kati yao ikiwa ni pamoja na dhamira ya kutaka kulivusha soka la Tanzania na kufikia hadi kubwa duniani.
Twissa pia ametoa mchanganuo wa sehemu ya fedha iliyoongezwa kutoka kiasi cha shuilingi billion 1.6 hadi billion 2.2 ambacho kitatumika kwa kila msimu hadi mwaka 2018.
Naye raisi wa shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi amesema ni faraja kwao kuona uhusiano wa kimaendeleo unapewa nafasi kati yao na kampuni ya mawasilino nchini Vodacom ambao wanaendelea kuonyesha dhamira ya dhati ya kulisaidia soka la Tanzania.
Hata hivyo malinzi akatoa angalizo kwa viongozi wa klabu za ligi kuu ambao wanadhamiria kuzitumia vibaya pesa zinazotolewa na wadhamini hao, tofauti na malengo yanayokusudiwa.
Kwa upande wa murugenzi mtendaji wa bodi wa ligi Boniface Wambura amesema kusainiwa kwa mkataba huo kunafungua mlango kwa vilabu kuwa na chachu ya kushindana zaidi kutokanana njaa waliyokua nayo ya muda mrefu kumalizwa na wadhamini wakuu.
Wambura pia ameahidi ligi bora kwa msimu ujao na wakati wowote kuanzia sasa watatoa ratiba ili kuwapa fursa viongozi na wachezaji kujitambua wataanza na nani na kumaliza na nani.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)





0 Comments