Naibu katibu wa Simba na Mjumbe wa kamati ya Utendaji wa Simba Collin Frisch hii leo amezindua Rasmi week ya Simba kwa
kubandika stika katika daladala na Taxi,kwa ajili ya kuwafahamisha watu juu ya Simba week,kabla ya kufikia kilele siku ya jumamosi Tarehe 8 Aug.2015 katika Simba Day.Uzinduzi huo umefanyika maeneo ya Posta Mpya jijini Dar es salaam.
![]() |
| Mjumbe wa kamati ya Utendaji wa Simba Collin Frisch hii leo amezindua Rasmi week ya Simba kwa kubandika stika katika Daladala na Taxi |
Akizungumza na Jamii na Michezo Collin Frisch amesema katika week hii yote wanachama na mashabiki wa Simba watakuwa wanajishughulisha na kazi za kijamii ikiwemo kutembelea watoto yatima.
Collin Frisch amesema katika week hii pia watafanya mambo mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa matawi,na kuwataka wapenzi wa simba kujitokeza na kujihusisha na shuguli mbalimbali za kijamii.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)










0 Comments