Ticker

6/recent/ticker-posts

VIDEO:ANGALI VIDEO YA PENALTI AZAM FC NA YANGA KOMBE LA KAGAME


Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY.30,2015 SAA 01:35 USIKU
AZAM FC imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya CECAFA Kagame Cupbaada ya ushindi wa penalty 5-3 baada ya sare
ya 0-0 ndani ya dakika 90.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, shujaa wa Azam FC alikuwa ni kipa Aishi Salum Manula aliyepangua penalti ya beki mpya wa kushoto wa Yanga SC, Mwinyi Hajji Mngwali.

Wachezaji Kipre Herman Tchetche, Serge Wawa Pascal wote raia wa Ivory Coast, John Bocco, Himid Mao na Aggrey Morris walifunga penati zao, wakati za Yanga SC zilifungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela na Godfrey Mwashiuya.  

katika mtanange wa dakika tisini Azam FC iliutawala mchezo hasa kipindi cha kwanza na kukosa magoli mengi kupitia kwa John Bocco, Kipre Tchetche na Shomari Kapombe.

ANGALI VIDEO YA PENALTI -AZAM FC NA YANGA

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments