Mabingwa wa Kenya Gor Mahia wamejisafisha katika ligi yao wenyewe huko Kenya, Baada ya kutopata ushindi dhidi ya Azam
Fc katika mashindano ya CECAFA ya mwaka 2015 ya klabu bingwa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Weekend hii Siku ya Jumapili, walimaliza unyonge kwa kuibamiza KCB,anayocheza kwa mkopo mchezaji wa Simba ya Tanzania Paul Mungai Kiongera, mabao 6-1 katika mchezo wa Ligi nchini Kenya uliofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Nyayo.
Mabao mawili ya Gor mahia yalifungwa na Michael Olunga ,na Meddie Kagere alifunga mawili pia,na bao lingine la Gor Mahia alifunga Khalid Aucho
Mlinzi wa KCB Mark Odhiambo alijifunga na kuisaidia Gor mahia Bao.
Huku Paul Kiongera akitumia vizuri makosa ya walinzi na kuipatia KCB bao la kufuta machozi.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments