Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:ANGALIA PARTY LA UBINGWA LA WA CAIRO BAADA YA KUNYAKUWA UBINGWA TANZANIA MASHINDANO YA KIKAPU

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 1,2015 SAA 10:14 JIONI
Cairo kutoka Misri imefanikiwa kutwaa ubingwa  wa mpira wa kikapu wa michuano ya majiji ya Afika Mashariki na Kati (East &
Central Africa Inter-Cities Championship) baada ya kuifunga timu ya Qardho ya Somalia.


Mchezo huo wa fainali uliopigwa jana kwenye uwanja wa ndani wa Taifa, timu ya Qardho ilifungwa kwa jumla ya vikapu 79 kwa 59 na Cairo kufanikiwa kutetea taji hilo ambalo walilitwaa pia mwaka uliopita.





Mashindano hayo yaliyohusisha Tanzania ambao walikuwa wenyeji, Kenya, Uganda, Somalia pamoja na Misri yalianza Mei 27 na Jana Mei 31 kumalizika huku timu za Tanzania zikishindwa kufanya vizuri katika mashindano hayo,na nafasi ya tatu kwa wavulana iliyochukuliwa na timu ya Tanzania Dar City kwa kuwachapa ndugu zao Dar Star kwa alama 77 kwa 64.

Kwa upande wa wanawake, timu ya Nairobi City imenyakua ubingwa baada ya kuifunga timu ya Kampala City kwa alama 77 dhidi ya alama 37.

ANGALIA PICHA MBALIMBALI 
























KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) 

Post a Comment

0 Comments