Mashindano ya mpira wa kikapu ya majiji yameendelea hii Leo katika uwanja wa ndani wa taifa kwa michezo ya nusu
fainali.
Nusu final ya kwanza kwa wanaume ilishuhudiwa timu ya Cairo kutoka misri ikiingia fainali baada ya kuifunga Dar city kwa alama 92 kwa 60.
Nusu fainali ya pili kwa wanaume timu ya Cardo imeshinda kwa alama 78 kwa 68 dhidi ya Dar star.kwa maana hiyo fainali kwa wanaume hapo kesho ni kati ya jiji la Cairo kutoka Misri na jiji la Cardo kutoka Somalia.
Kwa upande wa wanawake Nairobi na Dar es salaam,timu ya Nairobi ilishinda kwa vikapu 70 kwa 55.
Mchezo wa nusu fainali ya pili kwa wanawake timu ya Kcca ya Uganda imeshinda kwa alama 76 kwa 44 dhidi ya Dar city.
fainali kwa upande wa wanawake hapo kesho ni Kati ya jiji la Nairobi na Kcca kutoka Uganda.
ANGALIA PICHA MBALIMBALI
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)








0 Comments