Petr Cech amekuwa wa kwanza kusajilia na Arsenal katika dirisha hili la uhamisho baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea katika
klabu ya Chelsea siku ya jana Jumatatu alasiri.
Petr Cech amezungumza kwa mara yake ya kwanza kama mchezaji wa Arsenal,na amekubali kuwa katika Ligi Kuu England kuna changamoto inayosababishwa na wachezaji wakubwa,na timu kubwa zinapokutana kila wiki,huku pia akisisitiza Arsenal ni timu ambayo ilimpa changamoto kubwa na dhahiri matarajio yake ni kupata hamasa katika mechi.
Hata hivyo Petr Cech anaamini kuwa wakati huu amefanya uchaguzi mzuri kwenda Arsenal na anasema atakuwa na mafanikio akiwa katika klabu hiyo.
Petr Cech aliulizwa swali kuwa Baada ya kutumia miaka 11 ya mafanikio akiwa na Chelsea, ni lazima kuwe na uamuzi mgumu wa kuondoka?
"Ilikuwa pengine ni uamuzi mgumu nami kuondoka, lakini mwaka jana nikagundua kuwa mimi sikuwa katika wakati muafaka kwangu kukaa kwenye benchi. Nataka kucheza, nataka kuwa na nafasi ya kushindana kwa nafasi yangu katika timu na nataka kuwa sehemu manufaa kwa ajili ya timu na kufanya mambo mazuri kwenye uwanja ndani na nje.Natumaini na itabidi kuwe na uwezekano wa kushindana kwa nafasi yangu hapa Arsenal na natumaini kwamba naweza kuleta kitu cha ziada kidogo na timu ambayo inaweza kusaidia". alisema Petr Cech
KIPA Petr Cech ametambulishwa rasmi na Arsenal akitokea katika klabu ya Chelsea hapo jana, na amesaini mkataba wa miaka minne, unaotajwa kuwa na thamani ya Pauni Milioni 10 kwa mlinda mlango huyo hodari wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech.
Cech atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 100,000 kwa wiki,na anaweza akaidakia Arsenal kwa mara ya kwanza dhidi ya timu yake ya zamani Agosti 2 katika mchezo wa Ngao ya Jamii.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments