Ticker

6/recent/ticker-posts

MOURINHO:NIMERUDI NA KUWA BINGWA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.May .4,2015 SAA 09:19 MCHANA
Mourinho needs to bring through more youth, says Neville
Timu ya Chelsea ndiyo mabingwa wa ligi kuu ya England, baada ya kuifunga Crystal Palace bao 1-0 katika mchezo
uliofanyika katika uwanja wa Stamford Bridge. Bao la Chelsea lilifungwa katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza cha mchezo, likifungwa Eden Hazard.
Chelsea ilihitaji pointi tatu kutangazwa mabingwa wa ligi kuu ya England. Chelsea imetwaa ubingwa huo ikiwa bado na michezo mitatu, ikiwa imejikusanyia pointi 83 ikifuatiwa na mabingwa wa msimu uliopita Manchester City yenye pointi 70, huku Arsenal ikiwa katika nafasi ya tatu na pointi 67 na nafasi ya nne inakaliwa na Manchester United yenye pointi 65.
Ubingwa huo umemfanya kocha wa Chelsea Jose Mourinho ajisikie furaha, ajivune na kujisikia mchovu baada ya kazi ngumu ya kusaka taji hilo.
Ushindi huo umempa Mourinho ubingwa mara tatu akiwa kocha wa Chelsea, na kombe lake la kwanza akiwa kocha wa Chelsea mara baada ya kurejea mara ya pili kukiongoza kikosi hicho Msimu uliopita. Hili ni taji la tano kwa klabu hiyo na limekuja miaka mitano baada ya timu hiyo kuchukua kombe lake la mwisho, na ni miaka 60 tangu wachukue kombe la kwanza.
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho anasema kwamba nia yake aliporudi katika klabu ya Chelsea ilikuwa kufanya kazi kwa bidii na kuelekea kushinda ubingwa.
Eden Hazard celebrates after successfully following up his missed penalty
Mourinho alisema: "Nimerudi kufanya kazi na bora ambayo naweza na kuonesha kila kitu ambacho naweza ili kuwa mabingwa, ni matokeo yalikuwa kazi na kujituma. Wakati mimi narudi hapa nilijua kwamba nilikuja katika ligi ngumu sana kushinda katika ulimwengu wa soka. Na tumefanya hivyo.
Mourinho pia alifafanua alichokifanya baada ya ushindi
"Mimi nilikuwa na familia yangu tu nyuma benchi na naliweza kuwakumbatia na kuwabusu, basi wachezaji walifurahia uwanjani"

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments