Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:YAMETIMIA,YANGA MABINGWA WA LIGI KUU 2014-2015,...angalia picha mwanzo mpaka mwisho...

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.APRIL .27,2015 SAA 04:27 USIKU


Yanga bingwa wa ligi kuu Tanzania Bara 2014 - 2015 baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Polisi Morogoro mabao 4 - 1,katika
mchezo wa Ligi kuu uliopigwa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Yanga imenyakuwa Taji la 24 la ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kufikisha alama 55 ambazo ambazo haziwezwi kufikiwa na timu yeyote katika Ligi.
Kikosi cha Yanga kilichoanza

Kikosi cha Polisi Moro kilichoanza
Yanga imeivua Ubingwa Azam Fc ambao walikuwa wamiliki halali wa taji hilo msimu wa 2012-2013.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Amisi Tambwe ambaye alifunga mabao matatu Hat-Trick katika mchezo huo,bao la kwanza katika dakika ya 40, baada ya krosi safi ya Msuva.

Dk 53 Tambwe tena alifunga bao la pili kwa Yanga baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa, baada ya Msuva kupiga shuti kali.

 Dk 59 Tambwe aliifungia Yanga bao la tatu kwa kichwa baada ya kuiwahi krosi ya Ngassa.

Na Bao la Nne la Yanga lilipatikana Dk 66,ambapo Msuva alifunga bao hilo.

Dk ya 83, Admini Bantu alifunga bao la kufutia machozi la Polisi morogoro kwa shuti kali kutoka nje ya 18.

ANGALI PICHA ZA MCHEZO 









                      












                     







                    











                       







                         












                          












KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments