Vyanzo mbalimbali vya habari vya kuaminika ikiwemo sky sports vimeripoti kuwa mustakabali juu ya mkataba mpya
wa Raheem Sterling hautajadiliwa na Liverpool mpaka mwisho wa msimu.
Chanzo cha karibu na mshambuliaji huyo wa England kinasema kuwa mazungumzo yoyote juu ya mkataba mpya yatafanyika mpaka kipindi cha majira ya joto lakini anasisitiza kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kwa asilimia 100 ana nia ya kubaki katika klabu hiyo.
Mkataba wa Sterling unafikia kikomo mwishoni mwa msimu ujao na mapema mwezi uliopita meneja Brendan Rodgers alisema kuwa Anfield ndiyo mahali bora kwa ajili ya winga huyo mzaliwa wa Jamaica kuendeleza kazi yake,na kusisitiza kuwa klabu hiyo imemuandalia mkataba mnono mchezaji huyo.
"Najua katika kesi na Raheem ni kwamba atapewa ofa nzuri mno kwa mchezaji kijana ambaye ana miaka 20 na bado ana maendeleo," Rodgers alisema.
" alifanya baadhi ya hatua kubwa katika miaka michache iliyopita lakini kama nilivyosema sasa atapata tuzo yake kwa kuwa natumaini wawakilishi wake wanaweza kupatana mkataba na klabu hii".
"Mchezaji ana furaha sana na anataka kuendelea kufanya kazi kwa njia ambayo amekuwa". Rodgers alifafanua mapema mwezi uliopita.
Sterling alifunga bao lake la kwanza Kwa England katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Lithuania katika michuano ya kufuzu Ulaya siku ya Jumamosi iliyopita lakini atakosa hii leo Jumanne katika mechi ya kirafiki dhidi ya Italia katika mji wa Turin, baada ya kurudi Liverpool kufuatia kuumia kidole cha mguu.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments