Daniel Sturridge amejiunga na mchezaji mwenzake wa Liverpool Adam Lallana katika kujiondoa katika kikosi cha
England kutokana na kuumia, Chama cha soka FA kimetangaza.
Sturridge alijiunga na wachezaji wengine wa kikosi mjini Burton siku ya Jumatatu lakini sasa amerudi nyumbani baada ya kuwa nje katika kikosi cha mechi ya kufuzu michuano hiyo ya Ulaya dhidi ya Lithuania na mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alikuwa na matumaini ya kuonekana katika mechi yake ya kwanza na tangu walipofungwa dhidi ya Norway Septemba iliyopita wakati alipokuwa majeraha ambayo hayakumwezesha kucheza hadi mwisho wa Januari.
FA alithibitisha katika Taarifa ikisema: "mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge amewekwa kando katika kikosi cha England na amerudi nyumbani katika klabu yake siku ya Jumatatu jioni".
"Hii inafuatia kufanyiwa vipimo vya kuumia wakati Liverpool ikiwa katika mchezo dhidi ya Manchester United siku ya Jumapili".Taarifa ilifafanua.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments