Chama cha Soka England kimemshtaki beki wa Liverpool Martin Skrtel kufuatia mwenendo wa vurugu siku ya Jumapili
katika mchezo na Manchester United katika uwanja wa Anfield.
Kushtakiwa huku kunahusiana na tukio alilolifanya kwa kipa David De Gea kuelekea mwisho wa mchezo ambapo Skrtel alionekana kusimama juu ya mguu wa kipa huyo wa United.
Kama atapatikana na hatia, beki huyo wa Liverpool anaweza akakumbana na adhabu ya kupigwa marufuku michezo mtatu- adhabu sawa na aliyopewa mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, ambaye alipatikana na hatia ya kumkanyaga juu ya mguu beki wa Liverpool Emre Can wakati wa mchezo wa Capital One Cup dhidi ya Liverpool mwezi Januari.
kama Skrtel atapigwa marufuku michezo mitatu atakosa michezo muhimu ya Liverpool ya Premier League safari yao dhidi ya Arsenal Aprili 4, na mchezo wao wa Kombe la FA mechi ya marudiano dhidi ya Blackburn Aprili 8 pamoja na mchezo wa nyumbani dhidi ya Newcastle siku tano baadaye.
Liverpool tayari wanamkosa Steven Gerrard kwa michezo mitatu baada ya nahodha huyo wa klabu kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Ander Herrera.
Skrtel ana mpaka 6:00 Jumanne kujibu mashtaka hayo.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments